Saturday, 18 January 2014
wadudu kumbikumbi
Wengi wetu tumekuwa tukisikia kuwa kuna wadudu watamu sana na hupatikana
sana hasa katika msimu wa Mvua, wadudu hao ambao ni Maarufu kwa jina la
Kumbikumbi huanza kujitokeza wakati wa mvua hasa katika vichuguu vyao
vikubwa ambavyo hufaamika kwa kuishi wadudu wengine wanaojulikana kwa jina
la mchwa hawa hugeuka na kuja kuwa kumbikumbi.
Mkoa wa Mbeya ni moja ya maeneo ambayo kunapatikana kumbikumbi kwa wingi
sana .
Hiki ni kichuguu ambacho kimefunikwa kwa umahili kabisa.
Friday, 3 January 2014
UTALII WA ZIWA NYA
UNATANGAZA
UTALII WA NDANI: IFAHAMU HISTORIA YA ZIWA NYASA NA UNDANI WAKE.
Ziwa Nyasa (katika
Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya maziwa makubwa ya
Afrika ya Mashariki ikiwa na nafasi ya tatu baada ya Viktoria Nyanza na Ziwa
Tanganyika.
Lina urefu wa 560 km na
upana wa 50-80 km. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa
maji yake.
Mwonekano wa Jiwe
la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa
lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.
Jiwe la POMONDA
likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.
Kivutio kimoja wapo
katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda ni Machweo
ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali
Jiwe la POMONDA
lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina uwezo wa
kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa yanavyoonekana
pembeni mwa jiwe hilo.
Ufukwe wa Ziwa
Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli za
kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa Ziwa Nyasa au
kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa Nyasa.
Washiriki wa
Mdahalo wa Mabadiliko ya HAli ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa kwa
Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA
linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.
Hapo ni Meli ya MV
Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania kuelekea
Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyasa
Taarifa
zilizotolewa na Wazee waishio katika eneo la Mwambao wa Ziwa nyasa wamesema
kipimo cha ujazo wa Maji ya Ziwa Nyasa kujua yanapungua au yanaongezeka ni
alama hizo zinazoonekana mistari mieupe na rangi nyeusi kuwa ziwa limepungua
maji kwa kiasi kikubwa ambapo awali yalifikia katika mistari inayoonekana
kwenye jiwe hilo ewa
Kusini mwa ziwa unatoka
Mto Shire unaopeleka maji kwenye Mto Zambezi na hatimaye Bahari Hindi.
Kijiolojia ziwa ni sehemu
ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.
Eneo la ziwa ni 29,600
km². Sehemu kubwa ni eneo la Malawi, robo ya kusini-mashariki ni eneo la
Msumbiji, robo ya kaskazini-mashariki ni eneo la Tanzania. Lakini kuna ugomvi
kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mipaka. Malawi imedai ya kwamba maji yote
hadi ufukoni upande wa Tanzania ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Tanzania
imedai ya kwamba mpaka uwepo katikati kufuatana na uzoefu wa kimataifa.
Subscribe to:
Posts (Atom)