Saturday, 7 February 2015

Kuwasaidia Vijana Wakabiliane na Hali Ngumu

ULIMWENGU na mitindo yake hubadilika daima. Leo, mabadiliko hayo huonekana zaidi kwa sababu ya teknolojia ya kisasa. Kile kilichokuwa maarufu jana si kitu leo, na kinachopendwa leo, kesho kitakuwa kimepitwa na wakati. Mabadiliko hayo ya haraka yamewaathiri sana vijana.

Mabadiliko Makubwa ya Kijamii

Katika miaka ya karibuni, teknolojia imetokeza mabadiliko makubwa ambayo yamewaathiri sana vijana. Kwa mfano, katika nchi nyingi vijana huona simu za mkononi na kompyuta kuwa vyombo muhimu sana vya mawasiliano. Vituo vya kuwasiliana vimesababisha kuwe na mawasiliano mengi ambayo awali hayangewezekana. Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 19 nchini Australia anasema hivi: “Unaweza kuwa huna marafiki wowote, kisha mara moja uwe na marafiki chungu nzima kwenye Intaneti.”
Watu wengi wanakubali kwamba simu za mkononi na Intaneti zina manufaa mengi. Hata hivyo, watu wengi huona kwamba hawawezi kuishi bila vifaa hivyo. Profesa Donald Roberts wa Chuo Kikuu anasema kwamba wanafunzi fulani “hawawezi kumaliza dakika chache za mapumziko bila kutumia simu zao za mkononi.” Anasema hivi: “Ni kana kwamba hawawezi kutulia hadi wazungumze kwenye simu, ni kama wanasema ‘mbona kuna kimya kingi sana.’”
Vijana wengine wanakiri kwamba hawawezi kuishi bila vifaa hivyo. Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 16 aitwaye Stephanie anakiri hivi: “Mimi ni mraibu wa kutuma ujumbe wa haraka kupitia kompyuta na simu yangu ya mkononi, kwa sababu hiyo ndiyo njia kuu ya kuwasiliana na marafiki wangu. Ninaporudi nyumbani, mimi huenda moja kwa moja kwenye kompyuta na kutumia Intaneti mpaka saa tisa usiku.” Stephanie hulipa kati ya dola 100 hadi 500 kila mwezi kwa ajili ya gharama za simu. “Kufikia sasa, wazazi wangu wananidai zaidi ya dola 2,000 kwa sababu ya gharama za ziada za simu. Lakini nimezoea sana simu yangu ya mkononi hivi kwamba siwezi kufanya mambo yangu ya kawaida bila kuitumia.”
Kuna matatizo mengine zaidi ya pesa zinazotumika. Alipokuwa anafanya utafiti kuhusu maisha ya familia, Elinor Ochs, mtaalamu wa tabia na tamaduni za wanadamu aligundua kwamba mzazi aliporudi nyumbani kutoka kazini, mara nyingi mwenzi wake wa ndoa na watoto walikuwa wakijishughulisha tu na kile walichokuwa wakifanya hivi kwamba mara 2 kati ya 3 hata hawakumsalimu! Waliendelea tu kukazia fikira vifaa vyao vya elektroniki. Ochs anasema, “Tuliona pia jinsi ilivyo vigumu kwa wazazi kujihusisha katika utendaji wa watoto wao.” Anaongezea kusema kwamba utafiti huo ulipokuwa ukiendelea, wazazi walionekana wakijaribu kuepuka kuwasumbua watoto ambao walikuwa wakikazia fikira mambo waliyokuwa wakifanya.

Je, Kuna Madhara ya Kuwasiliana Kwenye Intaneti?

Wazazi na walimu wengi wanahangaishwa na muda ambao vijana wanatumia kwenye vituo vya Intaneti vya kuwasiliana. Vituo hivyo vya Intaneti humwezesha mtu kuanzisha kituo chake na kukiboresha kwa kuweka picha, video, na habari za kibinafsi.
Jambo linalowavutia watu kutumia vituo hivyo ni kwamba vinawawezesha kuwasiliana na marafiki. Vilevile kuanzisha kituo kama hicho humpa kijana nafasi ya kueleza maoni yake. Inaeleweka ni kwa nini vituo hivyo vinavutia sana vijana kwani kipindi cha kubalehe ni wakati ambapo kijana hujaribu kujielewa na kueleza hisia zake katika njia ambayo itawafikia na kuwagusa watu wengine.
Hata hivyo, tatizo moja linalozuka ni kwamba watu fulani hujifafanua kwa kutumia utu wanaotaka kuwa nao badala ya utu wao halisi. “Kuna kijana katika darasa langu ambaye anasema ana umri wa miaka 21 na anaishi Las Vegas,” anasema mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 15. Vijana hao wawili wanaishi kilomita 1,600 hivi kutoka Las Vegas.
Ni jambo la kawaida kwa watu kutoa habari za uwongo kama hizo. “Unaweza kufanya jambo lolote kwenye Intaneti,” anasema msichana Mwaustralia mwenye umri wa miaka 18. “Unaweza kujifanya kuwa mtu tofauti kabisa kwani hakuna mtu anayekujua. Unajihisi ukiwa na ujasiri. Unaweza kubuni mambo ili uonekane kuwa mtu mwenye kupendeza zaidi. Unaweza kuingiza picha zako ukiwa umevalia mavazi ambayo kwa kawaida hungevalia au ukifanya mambo ambayo kwa kawaida hungefanya. Unaweza kuandika mambo ambayo wewe mwenyewe huwezi kusema. Unahisi kwamba huwezi kulaumiwa kwa sababu huwezi kupatikana. Hakuna mtu anayekujua vizuri.”
Kama tu njia nyingine za mawasiliano, vituo vya Intaneti vya kuwasiliana vinaweza kuwa na manufaa au madhara. Je, wewe ukiwa mzazi unajua watoto wako wanafanya nini kwenye Intaneti? Je, unahakikisha kwamba wanatumia wakati wao vizuri?* (Waefeso 5:15, 16) Isitoshe, kutumia Intaneti vibaya kunaweza kumhatarisha kijana kwa njia mbalimbali. Baadhi ya njia hizo ni zipi?

Hatari za Kutumia Intaneti

Kwa kuwa watu wanaotumia Intaneti hawajitambulishi, watu wanaowavizia watoto ili hatimaye wafanye nao ngono huona Intaneti kuwa njia rahisi ya kuwanasa. Vijana wanaweza kunaswa bila kutarajia wanapotoa habari za kibinafsi kwenye Intaneti au wanapokubali kukutana na mtu ambaye wamekuwa wakiwasiliana naye. Watu fulani hudai kwamba “watoto hukabili hatari kubwa zaidi ya kufanyiwa ujeuri au kudhulumiwa ndani ya nyumba zao au mahali wanapochezea,” kinasema kitabu Parenting 911. “Hata hivyo, jambo linalowaogopesha wazazi wengi kuhusu watu wanaowavizia watoto ili wafanye nao ngono ni kwamba wanaweza kuingia nyumbani mwao kupitia Intaneti na kuwapotosha watoto wao.”
Teknolojia ya mawasiliano imetumiwa vibaya katika njia nyingine. Vijana wengine wametumia Intaneti ili kuwaonea wengine, kwa kuwadhihaki, kutoa maoni ya kuwabagua, kuwasumbua, au kuwatisha. Vituo fulani vimeanzishwa kwa kusudi la kumwaibisha mtu fulani, ilhali barua-pepe, vituo vya maongezi, na mitandao kama hiyo imetumiwa kuwachongea wengine. Msimamizi wa kikundi fulani cha kuangalia usalama kwenye Intaneti anaamini kwamba asilimia 80 hivi ya watoto kati ya umri wa miaka 10 hadi 14, wameathiriwa kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja na uonevu unaofanywa kwenye Intaneti.
Kwa kweli, uonevu si jambo jipya. Lakini sasa, uvumi, porojo, na uchongezi zinaweza kusambazwa mbali na kwa muda mfupi zaidi. Mara nyingi uonevu huo huwa mbaya zaidi. Katika visa fulani, simu za mkononi zilizo na kamera zimetumiwa kupiga picha na video zenye kuaibisha, labda mtu akiwa ndani ya chumba cha kubadili mavazi shuleni au ndani ya bafu. Kisha picha hizo huwekwa kwenye Intaneti na kutumwa kwa watu wanaotaka kuzitazama.

Jambo Linalozidi Kuhangaisha Jamii

Tatizo hilo lilisababisha Idara ya Sheria na Usalama wa Umma huko New Jersey, Marekani, kuwatumia wazazi na walezi barua iliyokuwa na himizo hili: “Tusaidieni kukabiliana na tatizo linalozuka la matumizi yasiyofaa ya Intaneti miongoni mwa watoto wakiwa ndani au nje ya shule.” Barua hiyo ilieleza waziwazi hangaiko la idara hiyo kuhusu kuweka habari za kibinafsi na picha kwenye Intaneti. Vituo vinavyotoa habari kama hizo huwavutia walaghai wawe vijana au watu wazima. Barua hiyo ilisema hivi pia, “Wazazi mnapaswa kujua kwamba mahangaiko haya ni ya kweli na mnaweza kuchangia sana kuwalinda watoto wenu kwa kujifunza mengi kuhusu Intaneti na kujua vituo ambavyo watoto wenu hufungua.”
Hata hivyo, wazazi wengine wanajua machache sana kuhusu yale ambayo watoto wao wanafanya kwenye Intaneti. Mama mmoja ambaye hufuatilia kwa ukaribu kile ambacho binti yake mwenye umri wa miaka 16 anafanya kwenye Intaneti anasema hivi: “Wazazi wanaweza kushtuka na kuaibika sana wakijua mambo ambayo watoto wao huweka na kuzungumzia kwenye Intaneti.” Kulingana na mtaalamu mmoja wa usalama kwenye Intaneti, vijana fulani huweka picha walizopigwa wakiwa wamevalia vibaya.

Madhara

Je, malalamiko hayo yanatoka kwa watu wazima wenye wasiwasi mwingi ambao wamesahau vituko vyao vya ujanani? Takwimu zinaonyesha hilo si kweli. Fikiria hili: Katika maeneo fulani, karibu asilimia 33 hivi ya wavulana na wasichana wenye umri wa miaka kati ya 15 na 17 wamewahi kufanya ngono. Zaidi ya nusu ya vijana wenye miaka kati ya 13 na 19 wanasema kwamba wamefanya ngono ya kinywa.
Je, teknolojia imechangia takwimu hizo zenye kushtua? Bila shaka. Ripoti moja katika gazeti New York Times Magazine inasema kwamba “simu za mkononi na Intaneti, ambazo huwawezesha vijana kufanya mambo bila kujulikana, hufanya iwe rahisi kwao kukutana na kufanya ngono bila kuwajibika.” Kwa kweli, inachukua muda mfupi sana kwenye kompyuta kupanga kukutana kwa siri na mtu wa jinsia nyingine. Katika uchunguzi mmoja, zaidi ya wasichana 4 kati ya 5 walikiri kwamba hawawi waangalifu sana wanapotumia Intaneti.
Watu wengine wanaotafuta mchumba au mtu wa kufanya naye ngono bila kuwajibika wamepata zaidi ya yale waliyotarajia. ‘Tumeshuhudia ongezeko la visa vya watu kulalwa kwa nguvu,’ anasema Jennifer Welch wa Idara ya Polisi ya Novato huko California. Anasema kwamba wahasiriwa wengi huwa wamewasiliana kwanza kupitia Intaneti na kukubali kukutana na watu ambao baadaye huwadhulumu.

Jihadhari na “Hekima ya Ulimwengu”!

Makala ya kuwashauri vijana katika magazeti hayachukui msimamo thabiti inapohusu vijana na ngono. Ingawa wanawatia moyo vijana kuwa safi kiadili au kujiepusha na ngono, lengo lao kuu ni kuwatia moyo wajihusishe na ngono “salama” badala ya kutojihusisha hata kidogo na ngono. Ni kama wanasema hivi: ‘Hatuwezi kuwazuia lakini angalau tunaweza kuwafundisha wawajibike.’
Kwenye makala iliyotolewa kwenye kituo kimoja cha Intaneti kinachoheshimika ambacho hutoa ushauri kwa vijana, suala la ama mtu anapaswa au hapaswi kufanya ngono lilitegemea mambo matatu: (1) hatari za kupata mimba, (2) hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, na (3) umuhimu wa kuamua kama msichana na mvulana wako tayari kihisia kufanya jambo hilo. “Lakini wewe ndiye utakayefanya uamuzi wa mwisho,” kinasema kituo hicho. Kilitaja kijuujuu tu kwamba mtu anapaswa pia kuzungumzia jambo hilo pamoja na mzazi wake. Makala hiyo haikutaja kama ni sawa ama si sawa kwa vijana kufanya ngono.
Ikiwa wewe ni mzazi, bila shaka ungependa watoto wako waongozwe na maoni bora zaidi kuliko “hekima ya ulimwengu” ambayo ni ya kipumbavu. (1 Wakorintho 1:20) Unaweza kuwasaidiaje wapite kipindi cha kubalehe na kuepuka hatari zilizozungumziwa katika makala hii? Jibu haliwezi kuwa tu kufunga kompyuta au kuwanyang’anya simu. Kusuluhisha mambo kijuujuu hakugusi mioyo. (Methali 4:23) Kumbuka pia kwamba huenda watoto wakawa wanatumia vifaa kama simu na Intaneti kutosheleza mahitaji fulani ambayo ukiwa mzazi unaweza kuyatosheleza kwa njia bora. Ni nini baadhi ya mahitaji hayo?
[Maelezo ya Chini]
Badala ya wazazi kushutumu Intaneti, wanapaswa kujua vituo ambavyo watoto wao hupenda kuvifungua. Kwa njia hiyo, watoto wanaweza kusaidiwa ‘kuzoeza nguvu zao za ufahamu kutofautisha yaliyo sawa na yaliyo makosa pia.’ (Waebrania 5:14) Mazoezi kama hayo kutoka kwa wazazi yatawasaidia watoto wanapokomaa.
[Blabu katika ukurasa wa 4]
“Ninaporudi nyumbani mimi huenda moja kwa moja kwenye kompyuta na kutumia Intaneti mpaka saa tisa usiku”
[Blabu katika ukurasa wa 5]
“Unaweza kufanya jambo lolote kwenye Intaneti. Unaweza kujifanya kuwa mtu tofauti kabisa kwani hakuna mtu anayekujua”
[Blabu katika ukurasa wa 7]
“Wazazi wanaweza kushtuka na kuaibika sana wakijua mambo ambayo watoto wao huweka na kuzungumzia kwenye Intaneti”
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 6]
Vituo vya Kuwasiliana—Simulizi la Msichana Mmoja
  “Nilianza kutumia kituo cha Intaneti cha shule yetu kuwasiliana na wanafunzi wenzangu na walimu. Nilianza kutumia saa moja kila juma kwenye kituo hicho. Baada ya muda nikaanza kukitumia kila siku. Nilikuwa nimenaswa sana hivi kwamba wakati ambapo sikuwa nikitumia Intaneti nilikuwa nikifikiria kuihusu. Sikuweza kukazia fikira kitu kingine chochote. Sikuweza kumaliza kazi yangu ya shuleni wala kukaza fikira nilipokuwa kwenye mikutano ya Kikristo, na hata niliwapuuza marafiki wangu. Mwishowe, wazazi wangu walitambua kilichokuwa kikiendelea nao wakaniwekea vizuizi. Ilikuwa vigumu kwangu kukubali vizuizi hivyo. Nilikasirika sana. Lakini sasa ninafurahi kwamba wazazi wangu walifanya hivyo nami nimefanya mabadiliko yanayofaa. Nisingependa kuhisi nimenaswa tena!”

Saturday, 6 December 2014

USHAURI; Jinsi Ya Kukuza, Kustawisha Na Kuendeleza Biashara


Moja ya changamoto kubwa kwenye biashara nyingi ni jinsi ya kuzikuza na kuendelea zaidi. Kuna biashara nyingi huku mitaani ziko vile vile miaka nenda miaka rudi. Pamoja na kuwepo hivyo hivyo kila mwaka bado wamiliki wa biashara hizi jawajapata mafanikio waliyotegemea kuyapata. Hili limekuwa tatizo kwa watu wengi sana na huenda ni tatizo ambalo limekusumbua wewe muda mrefu.
Kabla ya kuona ni jinsi gani unaweza kukuza, kustawisha na kuendeleza biashara yako naomba tuone alichoandika msomaji mwenzetu wa AMKA MTANZANIA.
Mimi ni mfugaji wa ng'ombe,mbuzi na kondoo pia nina duka la rejareja mwaka wa 3 sasa.Shida yangu ni namna ya kukuza ,kustawisha na kuendeleza biashara hii ya duka hadi kiwango cha kukidhi mahitaji ya wateja wote. Nimeplan mara nyingi kufikisha kiwango fulani cha mauzo mwisho nikifanya tathmini sijafikia ama nimeshuka kiwango.Naomba msaada ni mbinu zip nawezatumia kufikia lengo langu la kuikuza bishara.
Kama alivyosema msomaji mwenzetu hapo juu hii ni kiu ya wafanyabiashara wengi sana, jinsi ya kukuza biashara zetu.
Inawezekana unaweka mipango mizuri ila bado huoni matokeo mazuri. Kuna mambo mengi unaweza kufanya kukabili changamoto hii, hapa nitaeleza mambo manne ambayo unaweza kuanza kufanya na ukaona mabadiliko makubwa.
1. Weka malengo na mipango mizuri ya kufanikiwa.
Huu ndio mwanzo kabisa wa safari ya mafanikio katika jambo lolote unalofanya. Ila pia inawezekana umeshafanya hivi na bado umeshindwa kupata mafanikio. tatizo inakuwa nini?
Tatizo linaweza kuwa unaweka malengo yako vibaya au huweki mipango yako vizuri. Malengo na mipango unayoweka hakikisha inaeleza kwa kina kabisa ni kitu gani utafanya wakati gani na ni marekebisho gani unahitaji kufanya ili uweze kufanikiwa. Kusema tu labda baada ya miezi sita nataka nifikie mauzo ya milioni kumi haitoshi kukufikisha hapo. Ni lazima uchambue ni nini utabadili sasa ili uweze kufikia malengo hayo ya kuuza milioni kumi.
Kuna mambo mengi sana ya kurekebisha kwenye biashara hasa za reja reja ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Mambo kama jinsi unavyofanya biashara, muda unaofungua na kufunga, wafanyakazi unaoajiri, jinsi unavyochangamana na wateja na hata imani yako kwenye biashara yana nafasi kubwa sana kwenye mafanikio ya biashara yako. Hakikisha haya yamekaa vizuri kwanza kabla hujaona mafanikio makubwa kwenye biashara yako.
kitabu kava tangazo
2. Jua ni wapi unakosea na ufanye marekebisho haraka.
Kama unaweka malengo na mipango ila bado unashindwa kuifikia ni dhahiri kuna sehemu unakosea kwenye mipango yako au uteklezaji wa mipango yako. Na ili uweze kujua hilo ni lazima kila unaposhindwa kufikia lengo ujifanyie tathmini ya yote uliyofanya ili kujua ulikosea wapi. Sisi ni binadamu hivyo tunakosea mara nyingi sana, kitu kizuri ni kwamba tunapokosea ndipo tunapojifunza. Tumia makosa yako kama sehemu ya kujifunza ni njia ipi bora kwako kufikia malengo yako.
Sio kila mipango utakayokuwa nayo kwenye biashara yako itakuletea mafanikio. Jipime kila mara na jua ni mipango ipi inaleta mafanikio na ipi haileti mafanikio.
3. Kua wewe kwanza.
Moja ya sababu kubwa kwa nini biashara yako haikui ni kwa sababu wewe mwenyewe hukui. Biashara yako haiwezi kukua kama wewe mwenyewe hukui, sahau kabisa kuhusu hilo. Cha kushangaza asilimia kubwa ya watu wanataka biashara zao zikue wakati wao bado wako vile vile na wanafikiri vile vile, kitu ambacho hakiwezi kutokea. Wewe unakuaje? Unakua kwa kujifunza kuhusu biashara kupitia kujisomea vitabu, makala nzuri kama hizi, kuhudhuria mafunzo na hata semina mbalimbali. Kujua zaidi kuhusu wewe na biashara yako kukua soma; Hii ndio sababu kubwa kwa nini biashara yako haikui.
4. Epuka chuma ulete kwenye biashara yako.
Tatizo jingine kubwa kwenye mafanikio ya biashara zetu ni chuma ulete. Chuma ulete ameturudisha nyuma sana kwenye biashara zetu na wengine wamejikuta wakifunga biashara zao kabisa. Ubaya wa chuma ulete huenda mpaka sasa hujamjua vizuri na hivyo hutoweza kabisa kupambana naye. Nilishaandika kwa kirefu sana kuhusu chuma ulete na jinsi ya kupambana naye. Kusoma jinsi gani unaweza kuepuka chuma ulete bonyeza maandishi haya na kuielewa vizuri dhana ya chuma ulete na jinsi ya kujikomboa wewe na biashara yako jiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Kupata maelezo zaidi jinsi ya kujiunga bonyeza hayo maadhishi.
Kukua na kustawi kwa biashara yako ni jambo ambalo linawezekana vizuri sana kama utajua ni wapi unataka kwenda na utafikaje pale. Anza kufanya mambo hayo manne na utaona mabadiliko makubwa sana kwenye biashara zako.
Kwa ushauri zaidi wa kivitendo wa namna ya kuiondoa biashara yako hatua moja mpaka nyingine tafadhali wasiliana na mimi kwa mawasiliano hayo hapo chini.
Nakutakia kila la kheri katika safari hii ya mafanikio

Friday, 1 August 2014

Looking For 100,000$

A SACOOs based in Mbeya city, tanzania is looking for 100,000$ to source Women Entrepreneurs project.
I you would like to contribute or donate please call us at +255 766 46 10 68 or email us on mihingasime@gmail.com or cardinasime@yahoo.com


Saturday, 18 January 2014

wadudu kumbikumbi

Wengi wetu tumekuwa tukisikia kuwa kuna wadudu watamu sana na hupatikana sana hasa katika msimu wa Mvua, wadudu hao ambao ni Maarufu kwa jina la Kumbikumbi huanza kujitokeza wakati wa mvua hasa katika vichuguu vyao vikubwa ambavyo hufaamika kwa kuishi wadudu wengine wanaojulikana kwa jina la mchwa hawa hugeuka na kuja kuwa kumbikumbi. Mkoa wa Mbeya ni moja ya maeneo ambayo kunapatikana kumbikumbi kwa wingi sana . Hiki ni kichuguu ambacho kimefunikwa kwa umahili kabisa.
 

Friday, 3 January 2014

UTALII WA ZIWA NYA



UNATANGAZA UTALII WA NDANI: IFAHAMU HISTORIA YA ZIWA NYASA NA UNDANI WAKE.

Ziwa Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ikiwa na nafasi ya tatu baada ya Viktoria Nyanza na Ziwa Tanganyika.


Lina urefu wa 560 km na upana wa 50-80 km. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake.
Ziwa Nyasa linapatikana kati ya nchi za Malawi, Msumbiji na Tanzania.Description: https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjahxzZJ_mkg5tPTMN86kVkJYZHQC5Mp_8bsa8B8OzHaxYWKN498TRe5yDU_-QDD37MnZVmLAXSo_3Cvf1pD8LWNotvqYIBIREFzmqGbh4Cyw0Ws4TUkhZfY4OKUzOqnQb3ARvySwV8eQs8/s1600/N1.jpg
 Mwonekano wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.


 Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.
 Kivutio kimoja wapo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda ni Machweo ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali
 Jiwe la POMONDA lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina uwezo wa kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa yanavyoonekana pembeni mwa jiwe hilo.
 Ufukwe wa Ziwa Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli za kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa Ziwa Nyasa au kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa Nyasa.

 Washiriki wa Mdahalo wa Mabadiliko ya HAli ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.
 Hapo ni Meli ya MV Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania kuelekea Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyasa


 Taarifa zilizotolewa na Wazee waishio katika eneo la Mwambao wa Ziwa nyasa wamesema kipimo cha ujazo wa Maji ya Ziwa Nyasa kujua yanapungua au yanaongezeka ni alama hizo zinazoonekana mistari mieupe na rangi nyeusi kuwa ziwa limepungua maji kwa kiasi kikubwa ambapo awali yalifikia katika mistari inayoonekana kwenye jiwe hilo ewa 



Kusini mwa ziwa unatoka Mto Shire unaopeleka maji kwenye Mto Zambezi na hatimaye Bahari Hindi.
Kijiolojia ziwa ni sehemu ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.


Eneo la ziwa ni 29,600 km². Sehemu kubwa ni eneo la Malawi, robo ya kusini-mashariki ni eneo la Msumbiji, robo ya kaskazini-mashariki ni eneo la Tanzania. Lakini kuna ugomvi kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mipaka. Malawi imedai ya kwamba maji yote hadi ufukoni upande wa Tanzania ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Tanzania imedai ya kwamba mpaka uwepo katikati kufuatana na uzoefu wa kimataifa.



Monday, 23 December 2013

TUNATAMBUA UTALII WETU WA NDANI: TAZAMA SAFU ZA MILIMA YA LIVINGSTONE PAMOJA NA MIAMBA YA AINA YAKE PEMBEZONI MWA ZIWA NYASA!


Miamba pembezoni mwa ziwa nyasa Safu ya milima ya livingstone iliyoko mwambao wa ziwa nyasa Miamba iliyoko kata ya Lumbila ambako kihistoria ni wilaya ya kwanza kwa wakoloni iko wilaya ya Ludewa miamba ambayo ni vivutio kwa watalii wilayani ludewa mwambao wa ziwa nyasa. 

Have a look at beautiful natural beauties of Livingstone mountains around lake Nyasa. its memorable to visit there, try ti one day.


Uongozi mzima wa SHIRECOP co.ltd unawatiakia wasomaji wa blog hii heri na fanaka za X-mas na mwaka Mpya 2014